1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wafariki kwenye maandamano ya upinzani Senegal

17 Mei 2023

Watu watatu wamefariki dunia nchini Senegal baada ya makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, kufuatia mivutano iliyosababishwa na kesi inayomkabili kiongozi huyo.

https://p.dw.com/p/4RUp6
Ousmane Sonko
Picha: Fatma Esma Arslan/AA/picture alliance

Watu watatu wamefariki dunia nchini Senegal baada ya makabiliano kati ya polisi ya nchini humo na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko hapo jana kufuatia mivutano iliyosababishwa na kesi inayomkabili kiongozi huyo.

Wizara ya ulinzi ya Senegal inasema vijana wawili wamefariki dunia katika mji mkuu Dakar na katika mji wa kusini wa Zuguinchor afisa mmoja wa polisi amefariki baada ya kukanyagwa kwa bahati mbaya na gari la polisi wa kukabiliana na ghasia.

Kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP, makundi ya watu katika eneo la Zuguinchor ambalo Sonko ni Meya, waliwashambulia polisi kwa mawe huku polisi nao wakiwarushia mabomu ya kutoa machozi.

Sonko anatarajiwa kufika mahakamani leo ambapo anakabiliwa na madai ya ubakaji.