1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Afrika ya Kati

Watu watano wauawa na waasi wa CPC Jamhuri ya Afrika ya Kati

3 Novemba 2023

Watu watano wameuawa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya waasi wenye silaha wa CPC, kushambulia mji wa Kaskazini Magharibi wa Moyenne Sido unaopakana na Chad.

https://p.dw.com/p/4YM3z
Jeshi, likisaidiwa na vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Wanajeshi wa Urusi na Rwanda, wamekuwa wakipambana na kundi la CPC kwa miaka mingi.
Jeshi, likisaidiwa na vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Wanajeshi wa Urusi na Rwanda, wamekuwa wakipambana na kundi la CPC kwa miaka mingi.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Meya wa mji huo Salomon Yamindji amesema waasi hao wapatao 300 walivamia majira ya alfajiri.

Manusura mmoja alithibitisha idadi ya waliofariki na kusema mmoja wao alikuwa ni mwanamke. CPC walitoa taarifa hapo baadaye na kudai kuudhibiti mji huo na kutoa wito kwa wakazi kujiunga nao.

Jeshi halijatoa tamko lolote.

Wanamgambo wa CPC wanalenga kupindua matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka 2020 ambao ulimrejesha madarakani Rais Faustin-Archange Touadera kwa muhula wa pili.

Jeshi, likisaidiwa na vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Wanajeshi wa Urusi na Rwanda, wamekuwa wakipambana na kundi hilo kwa miaka mingi.