1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Watu watano wamekufa Pakistan katika shambulio la bomu

3 Novemba 2023

Watu watano wamekufa akiwemo afisa mmoja wa polisi na wengine 20 wamejeruhiwa kaskazini Magharibi mwa Pakistan baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwenye pikipiki kuripuka

https://p.dw.com/p/4YNtr
Rais wa Pakistan Arif Alvi
Rais wa Pakistan Arif Alvi Picha: Mehmet Eser/AA/picture alliance

Bomu hilo liliripuliwa karibu na kituo cha basi kinachotumiwa na watu wengi.

Afisa wa polisi Gul Sher Khan amesema shambulio hilo lililokuwa linawalenga maafisa wa Polisi, lilitokea huko Dera Ismail Khan katika mji wa Khyber mkoa wa Pakhtunkhwa unaopakana na Afghanistan.

Watu sita wauwawa kwa risasi Pakistan

Hadi sasa hakuna kundi lolote lilitaja kuhusika na tukio hilo lakini linashukiwa kundi la Taliban huko Pakistan, ambalo limekuwa likizidisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama tangu mwaka 2022.

Mamlaka ya Islamabad imesema kundi hilo limeimarika tangu Taliban walipochukua mamlaka huko Afghanistan mwaka 2021.