Takriban watu 40 wameuwawa eneo la mpaka wa Sudan
5 Februari 2024Takriban watu 40,wengi wao wakiwa raia wa kawaida wameuwawa katika machafuko yaliyotokea kwenye eneo linalozozaniwa la mpakani baina ya Sudan Kusini na Sudan.
Mapigano hayo yametokea mwishoni mwa Juma na kusababisha mamia ya watu kukimbilia usalama katika kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa,kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa leo na afisa mmoja wa serikali.
Mapigano yameshuhudiwa mara kwa mara katika mkoa wa Abyeiyakiyahusisha makundi mawili yanayohasimiana ya jamii ya Kabila la Dinka. Uhasama baina ya makundi hayo unatokana na mvutano wa mpaka, unaoamua juu ya mapato ya kodi yanayokusanywa kutokana na biashara ya kuvuka mpaka huo.
Taarifa pia zinasema watu wengine 18 waliuwawa jana Jumapili katika tukio jingine tofauti kwenye eneo hilo.