1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalawi

Wanne wafariki katika msafara wa mazishi ya hayati Chilima

17 Juni 2024

Watu wanne wamekufa na wengine 12 wamejeruhiwa baada ya gari lililokuwa kwenye msafara wa hayati makamu wa rais wa Malawi kupoteza mwelekeo na kuwagonga waombolezaji katika kijiji cha Ntcheu, katikati mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4h75L
Malawi | Miili ya makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima ikipakiwa kwenye ndege kwa ajili ya kusafirishwa
Miili ya makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima ikipakiwa kwenye ndege kwa ajili ya kusafirishwaPicha: Zambia Air Force via REUTERS

Polisi imesema gari hilo lilikuwa sehemu ya msafara wa magari uliokuwa ukiusafirisha mwili wa hayati Saulos Chilima, aliyefariki katika ajali ya ndege ya kijeshi wiki iliyopita.

Gari hilo, pamoja na magari mengine ya kijeshi, polisi na ya raia, yalikuwa yakielekea kijiji alichozaliwa Chilima, kilomita 180 kusini mwa mji mkuu Lilongwe, kwa ajili ya mazishi yake leo Jumatatu - ambayo imetangazwa kuwa siku ya mapumziko.

Soma pia: Chilima kupewa heshima ya mazishi ya kitaifa nchini Malawi 

Maelfu ya watu walijitokeza barabarani kuona jeneza la makamu huyo wa rais.

Mashuhuda wameliambia shirika la habari la AFP kuwa, gari hilo liliwagonga waombolezaji baada ya kupoteza mwelekeo.