SiasaSudan
Watu tisa, wakiwemo askari wanne, wameuawa Sudan
24 Julai 2023Matangazo
Mapigano hayo yamesababisha mamilioni ya watu kunasa majumbani mwao na baadhi wakiwa bila ya maji, hasa katika viunga vya mji mkuu Khartoum ambako wakaazi wanatoa wito wa misaada ya chakula ili kuwasaidia kuishi.
Katika mji wa Port Sudan, pwani ya mashariki ambayo kwa kiasi kikubwa imenusurika vita hivyo mpaka sasa,jeshi limesema mtoto alinusurika ajali ya ndege aina ya Antonov ambayo iliwauwa watu wengine tisa.
Soma pia:Sudan yatimiza siku 100 za mapigano
Uwanja wa ndege wa Port Sudan ndio wa pekee unaondelea kufanya kazi nchini humo kutokana na mgogoro wa kivita.