Watu sita wauwawa kwa risasi Pakistan
14 Oktoba 2023Matangazo
Akitoa taarifa ya tukio hilo mapema leo, Afisa wa polisi katika eneo hilo Hidayatullah Dasgti amesema, watu hao wenye silaha walifyatua risasi usiku kucha wakizielekeza kwa mafundi nane wa ujenzi katika mji wa Turbat ulio kilometa 606 kusini mwa mji mkuu wa mkoa wa Baluchistan, Quetta. Watu wawili wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kwa kuhusika na tukio hilo. Kwa miongo miwili sasa, Baluchistan pamekuwa eneo la matukio ya uasi wa kiwango cha chini unaofanywa na jeshi la ukombozi la Baluchistan pamoja na makundi mengine ya wanaotaka kujitenga, wakidai uhuru kutoka kwa serikali kuu ya mjini Islamabad. Mara nyingi waasi hao huwalenga watu kutoka Punjab.