1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu sita wauawa Nigeria

Isaac Gamba
27 Desemba 2016

Kiasi ya watu sita wameuawa katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria, wakati wafugaji wakishukiwa kufanya shambulizi katika maeneo ya jimbo hilo.

https://p.dw.com/p/2UuY8
Nigeria Unruhen und Landwirtschaft
Picha: AFP/Getty Images

Mmoja wa wabunge wa zamani nchini humo, Gideon Morik, amethibitisha taarifa hizo hapo jana.  Mapigano yaliyochukua muda mrefu kuwania ardhi na haki za maeneo ya malisho kwa ajili ya mifugo, yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika maeneo ya katikati na kaskazini mwa Nigeria. Mbunge huyo alithibitisha kuuawa kwa watu hao sita akiwemo binti yake mwenye umri wa miaka 17, ambaye alikuwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya kumaliza elimu yake ya sekondari. Aliongeza kuwa washambuliaji hao waliwajeruhi watu wengi na kuharibu nyumba kadhaa kabla ya kutoweka.  Gavana wa jimbo hilo, Nasri El- Rufai, amelilaani shambulizi hilo.