1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUturuki

Watu sita wakutwa hai baada ya kunasa katika kifusi Uturuki

10 Februari 2023

Watu sita wameokolewa wakiwa hai chini ya vifusi nchini Uturuki, huku idadi ya vifo ikipindukia 21,000, kutokana na tetemeko la ardhi.

https://p.dw.com/p/4NK29
Türkei Erdbeben Gaziantep | Rettung von Adnan Mohammet Korkut
Picha: IHA via AP/picture alliance

Watu sita wameokolewa wakiwa hai nchini Uturuki kutoka katika kifusi, ikiwa zadi ya masaa 101 baada ya kutokea tetemeko la ardhi ambalo limegharimu maisha ya zaidi ya watu 20,000.

Kwa mujibu wa mmoja wa maafisa wa uokozi Murat Baygul manusura walikuwa wamekumbatiana katika sehemu iliyosalia kwenye upenyo wa jengo lililoporomoka.

Mapema Jumatatu tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lilikumba eneo la mpakani kati ya Uturuki na Syria, eneo ambalo lina wakazi zaidi ya milioni 13.5.