Watu kumi wauwawa kwenye shambulio la bomu Lebanon
25 Januari 2008Matangazo
Watu takriban 10 wameuwawa leo nchini Lebanon kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Wakristo mjini Beirut. Bomu hilo liliilenga gari la afisa wa polisi wa cheo cha juu.
Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika hujuma hiyo iliyofanywa siku kumi baada ya bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari kuiharibu gari ya Marekani mjini Beirut. Watu watatu waliuwawa na wengine 16 kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Lebanon imekumbwa na mashambulio ya mabomu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, mengi yakiwalenga wanasiasa wanaoipinga Syria pamoja na waandishi wa habari.