Watu kadhaa waliuwawa DRC mnamo mwezi Septemba
1 Novemba 2018Matangazo
Ofisi ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema makundi yenye silaha pamoja na majeshi ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamefanya mauaji ya watu 92 mwezi Septemba.
Ofisi ya pamoja ya Umoja wa mataifa kwa ajili ya haki za binadamu imerekodi matukio 623 ya ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati mwezi uliopita , ikiwa ni ongezeko kutoka matukio 620 mwezi Agosti na matukio 515 mwezi Julai.
Ofisi hiyo imeongeza kwamba asilimia 48 imefanywa na wapiganaji kutoka makundi ya watu wenye silaha, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiasi watu 67.