1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadhaa wakamatwa kuhusiana na mgogoro wa usalama Amhara

5 Agosti 2023

Mamlaka nchini Ethiopia imewakamata watu kadhaa wanaohusishwa na mgogoro wa usalama katika jimbo la Amhara. Ni muda mfupi baada ya serikali kutangaza hali ya hatari.

https://p.dw.com/p/4UoTa
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Mesay Tekelu/DW

Amri hiyo ya hali ya hatari iliyotolewa na serikali ilitokana na mapigano kati ya wanamgambo wa ndani ya jimbo la Amhara na vikosi vya jeshi la serikali. Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed pia imesema kwamba hatua za dharura zimewekwa katika jimbo la Amhara kwa muda wa miezi sita lakini amri ya hali ya hatari inaweza kuwekwa katika nchi nzima iwapo serikali italazimika kufanya hivyo kwa kuzingatia hali au harakati zozote zikazoashiria kutishia usalama wa nchi.

Soma zaidi: Ethiopia yatangaza hali ya dharura

Mapigano yameongezeka katika wiki za hivi karibuni katika eneo la Amhara, na yamesababisha serikali za kigeni kuwataka raia wao waondoke kutoka kwenye eneo hilo wakati ambapo mashirika ya ndege yamesitisha safari kwenda katika jimbo la Amhara.