1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 80 wauawa katika shambulio la RSF nchini Sudan

16 Agosti 2024

Takriban watu 80 wameuawa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na kikosi cha wanamgambo nchini Sudan RSF katika kijiji cha kusini mashariki mwa nchi hiyo. Hayo yameelezwa na chanzo kimoja nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jYwA
Sudan | Vorsitzender des Souveränen Rates des Sudan | Abdel Fattah al-Burhan
Picha: AFP

Shambulio hilo limetokea jana Alhamisi katika kijiji cha Jalgini kwenye jimbo la Sennar.

Chanzo katika kituo cha matibabu cha Jalgini kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa jana Alhamisi walipokea miili 55 na makumi ya wengine waliojeruhiwa.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa watu 25 wengine wamefariki leo na kufikisha idadi jumla ya waliopoteza maisha kufikia watu 80.

Mmoja wa manusura amesema vikosi vya RSF ndio vilivyohusika na hujuma hiyo.

Shambulio hilo limefanyika wakati mazungumzo yaliyofadhiliwa na Marekani yanayolenga kuvimaliza vita vya miezi 16 kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha ESF yanaendelea mjini Geneva.