1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Watu 8 wameuwawa katika ufyetuaji risasi Afrika Kusini

5 Juni 2023

Watu wenye silaha mwishoni mwa juma walivamia makaazi ya muda ya wanaume karibu na mji wa Durban, ulioko kusini mashariki mwa Afrika Kusini na kuwauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine wawili.

https://p.dw.com/p/4SCqO
Südafrika | Schüsse in einer Bar in Soweto mit mindestens 15 Toten
Picha: Ihsaan Haffejee/AFP/Getty Images

Hayo yaliarifiwa na polisi jana Jumapili ikielezwa kwamba ni tukio la hivi karibuni kabisa la mashambulio ya ufyetuaji risasi nchini humo. Watu saba walitangazwa kufariki hapo hapo baada ya tukio hilo lililotokea Jumamosi katika mtaa wa Umlazi, mtu wa nane alifariki jana Jumapili.

Soma pia: Sudan Kusini inakabiliwa na mgogoro wa kibinadamu

Polisi imeeleza kwamba wanaume 12 walikuwa ndani ya chumba kimoja wakinywa pombe na ghafla watu wenye silaha waliwavamia na kuwapiga risasi na kisha kukimbia.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi 10 zenye idadi kubwa ya matukio ya mauaji ya kukusudia duniani na katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo imekuwa ikiripoti visa vingi vya mashambulizi ya ufyetuaji risasi yanayowalenga watu wengi.