1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu 72 wafa maji Ufilipino wangi wao katika Pasaka

10 Aprili 2023

Watu 72 wamekufa kwa kuzama kwenye maji tangu mwanzo mwa mwezi huu, huku rekodi ikonesha vifo vingi zaidi vimetokea katika kipindi hiki cha mapunziko ya siku za Sikukuu ya Pasaka.

https://p.dw.com/p/4Ps6J
Philippinen der tropische Wirbelsturm Kompasu verursacht Hochwasser
Picha: Philippine coast guard via REUTERS

Watu 72 wamekufa kwa kuzama kwenye maji tangu mwanzo mwa mwezi huu, huku rekodi ikonesha vifo vingi zaidi vimetokea katika kipindi hiki cha mapunziko ya siku za Sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi la Ufilipino, Kanali Jean Fajardo, rekodi ya vifo 67 inajumuisha matukio ya kuanzia Aprili Mosi hadi Jumapili ya Pasaka, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Amesema watu wengi walifurahishwa na kutembelea maeneo mazuri ya fukwe, huku baadhi ya vifo vilihusisha watoto walioachwa bila ya uangalizi, vingine ulevi na wengine mikasa ya kusukumana wenyewe kwa wenyewe kwenye maji.

Vifo vitokanavyo na kuzama kwenye maji vinachukua nafasi ya tatu duniani. Shirika la Afya Duniani linakadiria watu 236,000 wanakufa kila mwaka duniani kutokana na mikasa hiyo.