1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 7 wauawa kutokana na shambulio la taliban karibu na Islamabad.

Abdu Said Mtullya9 Juni 2010

Taliban washambulia msafara wa magari karibu na Islamabad.

https://p.dw.com/p/NlvO
Msafara wa magari ya NATO ulioshambuliwa na Taliban.Picha: AP

Msafara wa magari yaliyokuwa yanapeleka mahitaji kwa ajili ya majeshi ya nato yaliyopo Afghanistan umeshambuliwa, na watu saba wameuawa.Habari zaidi zinasema washambuliaji pia waliyachoma moto malori na magari kadhaa ya kijeshi.

Polisi ya Pakistan imearifu kuwa shambulio hilo lilitokea jana usiku karibu na mji wa islamabad.Mku wa polisi wa mji huo Kalim Imam amesema washambuliaji wapatao 12 waliokuwa wamepanda mapikipiki na gari aina ya pickup waliyashambulia malori na matamki ya mafuta .Afisa mwengine wa polisi aliarifu kuwa malori 20 pamoja na magari ya deraya 80 yaliteketezwa. Amesema magari zaidi ya 80 yalikuwa yameegeshwa wakati wa shambulio hilo.

Wazima moto walihitaji saa nyingi ili kuweza kuizima myoto-Dereva mmoja wa lori aliwaambia wasndishi wa habari kwamba alikuwa amelala ndani ya lori lake, na aliamshwa na milio ya bunduki. Dereva huyo alisema kuwa aliruka kutoka kwenye lori na kuwaona watu wakishambulia.

Mkurugenzi wa kitengo cha dharura kwenye hospitali ya taasisi ya sayansi ya tiba, Mohammed Naser amesema maiti saba ziliondolewa kutoka kwenye sehemu palipotokea shambulio. Watu wengine watano walijeruhiwa.Mkurugezi huyo ameeleza kuwa uchunguzi uliofanywa umebainisha kwamba watu wanne walikufa kutokana na majeraha ya risasi na mmoja aliungua moto kabisa.

Wapiganaji wa kitaliban mara kwa mara wanayashambulia malori yanayopeleka mafuta na mahitaji mengine kwa ajili ya majeshi ya Nato yaliyopo Afghanistan.

Misafara ya magari inayopeleka mahitaji hayo huanzia kwenye mji wa bandari wa Karachi nchini Pakistan.Lakini hadi sasa idadi kubwa ya mashambulio hayo yamefanyika katika jimbo la Khyber-Pakhtunkhwa kaskazini magharibi mwa Baluchistan.

Lakini shambulio la jana usiku ni la kwanza kufanywa na taliban karibu na mji wa Islamabad. Wapiganaji wa Taliban na wa alkaida wameimarisha mashambulio ya kujitoa mhanga na ya aina nyingine katika sehemu za serikali na za raia ili kulipiza mashambulio yanayofanywa na majeshi ya Nato kwenye ngome za viongozi wa makabila katika eneo la mpaka wa Afghanistan.

Watu zaidi 3500 wameshauawa kutokana na mashambulio hayo tokea katikati ya mwaka 2007.

Mwandishi/Mtullya Abdu.

Mhariri/Othman Miraj