Janga
Watu 4 washitakiwa kwa kuhusika na shambulio la Moscow
25 Machi 2024Matangazo
Taarifa ya mahakama imesema washukiwa wawili kati ya hao wanne wamekiri kuhusika na shambulio hilo baada ya kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Basmanny ya mjini Moscow. Mmoja miongoni mwao ana umri wa miaka 19.
Watu wanne washitakiwa kwa shambulizi la Moscow lililouwa zaidi ya watu 130
Watuhumiwa hao wametakiwa kujibu mashtaka juu ya kufanya hujuma ya kigaidi na kusababisha vifo vya watu.
Wakati huo huo Urusi inaendelea kuomboleza vifo vya watu waliouliwa na washirika wa rais Vladmir Putin wanamtaka afikirie kurejesha adhabu ya kifo kwa magaidi na wauaji.