1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMali

Watu 31 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Mali

28 Februari 2024

Watu 31 wamekufa na wengine 10 wamejeruhiwa baada ya basi walimokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto karibu na mji wa magharibi wa Kenieba, nchini Mali.

https://p.dw.com/p/4cxiN
Basi limeharibika kabisa baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani
Basi limeharibika kabisa baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabaraniPicha: Cheikh Dieng/AFP

Wizara ya uchukuzi nchini Mali imesema katika taarifa kuwa, basi hilo lilikuwa linaelekea Burkina Faso wakati ajali hiyo ilipotokea majira ya saa kumi na moja jioni.

Wizara hiyo ya uchukuzi imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva kushindwa kulidhibiti basi.

Soma pia:  ECOWAS yaziondolea vikwazo Guinea, Mali

Matukio ya ajali za barabarani ni kawaida katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi ambapo sekta ya uchukuzi wa umma imelemewa pamoja na kuwepo ukaguzi duni wa mabasi ya kubebea abiria.

Mwaka uliopita, takwimu za Umoja wa Mataifa zilionyesha kuwa bara la Afrika limeshuhudia robo ya vifo vilivyotokana na ajali za barabarani duniani licha ya bara hilo kuwa na asilimia mbili pekee ya magari kote duniani.