JamiiChina
Watu 29 wafariki katika ajali ya moto kwenye hospitali China
19 Aprili 2023Matangazo
Naibu mkuu wa huduma za zima moto mjini Beijing amesema yumkini moto huo ulisababishwa na shughuli za ukarabati zilizokuwa zikifanyika katika hospitali hiyo. Miongoni mwa waliokamatwa ni mkuu wa hospitali ya Changfeng na maafisa wawili wa kampuni ya ujenzi iliyohusika.
Huduma za wazimamoto zimefanikiwa kuwaoka wagonjwa 142 kutoka kwenye jengo la hospitali hiyo lililokuwa likiwaka moto na kuwahamishia katika ituo vingine vya matibabu.
Ripoti za vyombo vya habari zimeeleza kuwa wengi wa waliouawa ni vikongwe waliokuwa wamelazwa hospitalini wakiwa hawana nguvu za kukimbia. Serikli imeamuru ukaguzi wa kiusalama katika hospitali zote baada ya ajali hiyo.