1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 22 wauawa Rafah kufuatia mashambulizi ya Israel

22 Aprili 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi katika mji wa Rafah na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 22, huku 18 kati yao wakiwa ni watoto.

https://p.dw.com/p/4f286
Gaza | Mashambulizi ya Israel huko Rafah
Vikosi vya ulinzi wa raia pamoja na wakaazi wa Rafah wakiwa kwenye shughuli za utafutaji na uokoaji baada ya shambulio la Israel mnamo Aprili 04, 2024.Picha: Jehad Alshrafi/Anadolu/picture alliance

Eneo hilo la kusini mwa Ukanda wa Gaza huwahifadhi karibu nusu ya wakazi milioni 2.3 ambao walimbia machafuko katika maeneo mengine.

Hayo yanajiri wakati Baraza la Wawakilishi la Marekani liliidhinisha kitita cha dola bilioni 13 za msaada wa kijeshi kwa Israel ambayo ni mshirika wa kihistoria wa Marekani. Hata hivyo Bunge hilo liliidhinisha pia karibu dola bilioni 9 za msaada wa kibinadamu kwa Gaza.

Soma pia: Israel yaendelea kuulenga mji wa Rafah, Ukanda wa Gaza

Kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas limelaani hatua ya mpango mpya wa msaada kwa Israel, ambao kwa kiasi kikubwa utaimarisha mifumo yake ya ulinzi wa angani na kusema kuwa msaada huo unakiuka sheria za kimataifa na ni idhni kwa serikali ya Israel kuendeleza vita vyake.