Watu 200 wakamatwa maandamano ya ongezeko la kodi Kenya
19 Juni 2024Mashirika ya kiraia yamesema maandamano hayo na mpango wa waandamanaji kukaa nje ya majengo ya bunge utaendelea licha ya kukamatwa kwa waandamanaji 210.
Kamanda wa Polisi wa Nairobi, Adamson Bungei, amesema hakuna kundi lolote lililopewa kibali cha kufanya maandamano katika mji mkuu huo, licha ya kwamba Wakenya wamehakikishiwa haki ya kuandamana kwa amani katika katiba.
Soma zaidi: Waandamanaji wakamatwa Kenya wakipinga muswada wa fedha
Bungei alisema waandaaji wa maandmano wanatakiwa kuwaarifu polisi mapema, kitu ambacho hawakufanya.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaza mamia ya waandamanaji siku ya Jumanne (Juni 18), hali iliyowalazimisha wafanyabiashara kufunga biashara zao kwa muda kwa kuhofia mali zao kuporwa.
Baadhi ya mapendekezo ya kuongeza ushuru katika mswada huo yalitupiliwa mbali siku ya Jumanne, baada ya wabunge wa chama tawala kufanya mkutano na Rais William Ruto.