1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 185 wauawa katika mapigano kati ya Boko Haram na jeshi la Nigeria

Admin.WagnerD22 Aprili 2013

Watu 185 wameripotiwa kuuawa na wengine 2000 kuachwa bila makaazi, baada ya kutokea mapigano makali kati ya Jeshi na wanaoshukiwa kuwa waasi wa Kiislamu katika eneo la Baga, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/18Ka3
In this image shot with a mobile phone, a young girl stands amid the burned ruins of Baga, Nigeria, on Sunday, April 21, 2013. Fighting between Nigeria's military and Islamic extremists killed at least 185 people in a fishing community in the nation's far northeast, officials said Sunday, an attack that saw insurgents fire rocket-propelled grenades and soldiers spray machine-gun fire into neighborhoods filled with civilians.(AP Photo/Haruna Umar) pixel
Nigeria Baga Kämpfe mit Boko Haram 21.04.2013Picha: picture alliance/AP Photo

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Gavana wa eneo hilo Kashim Shettima,amesema kuwa Mapambano hayo yametokea katika kijiji cha Baga kinachotumika kwa shuguli za uvuvi katika ziwa Chad na kusababisha nyumaba kadhaa kuchomwa moto na watu 2000 kuachwa bila makazi

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck JonathanPicha: picture-alliance/dpa

Msemaji wa Jeshi la Nigeria katika mjini wa Borno Lt.Colonel Sagir Musa ameliambia shairika la habari la AFP kwamba vyombo vya habari vimeripoti kuwa zaid ya watu 180 wanatajwa kufariki katika tukio hilo kubwa.

Duru za habari kutoka katika eneo hilo,zinaripoti kuwa mapigano hayo yametokea wakati jeshi la Nigeria lilipo jaaribu kuzunguka msikiti mmoja ili kuwatafuta baadhi ya wapiganaji wa kislaamu wanaoshukiwa na jaeshi hilo.

Mapigano hayo yemsababisha wananchi wa kijiji hicho kukimbia makazi yao baada ya kuzuka mapambanao hayo kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kiislamu na hadi sasa hakuna taarifa ya kurejea katika maeneo yao.

Licha ya kuwa hakuna alama yoyote ya kuaonesha kuwapo na uharibifu mubwa katika kijiji hicho, lakini serikali ya Nigeria imeshindwa kutaja idadi kamili ya watu waliouawa katika mapigano hayo hadi sasa ,huku kukiwa na taarifa kwamba watu 185 wamepoteza maisha.

Hadi sasa hakuna taarifa yoyote iwapo waasi hao ni kutoka katika kundi la Boko Hara,mingawa Jeshi la Nigeria limekuwa na historia ya mapambano ya muda mrefu na wapiganaji wa kiisalamu wa Boko Haram,waliopo katika mji wa Borno,mapigano ambayo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha yao.

Kazi ya Kundi la Boko Haram mji wa Maiduguri
Kazi ya Kundi la Boko Haram mji wa MaiduguriPicha: APImages

Utawala wa kiislaamu unahitajika.

Kundi la Boko Haram limesema kuwa hayo ni mapambano ya kutafuta utawala wa kiislamu nchini Nigeria katika eneo la waislamu wengi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kundi la Boko Haram linautumia mji wa Borno ambao ni mji mkuu wa Maiduguri kama ngome yao licha ya kuwa jeshi la Nigeria limekuwa likiwafukuza kutoka katika mji huo na kwenda pembeni ya mji huo.

Hadi sasa inakadiriwa watu 3,000 wameuawa katika mapigano nchini Nigeria tokea mwaka 2009,ikijumuisha mauaji yanayofanywa na vyombo vya usalama na kutuhumiwa kwa kuvunja haki za binadamu na mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa.Nigeria ni nchi yenye wakaazi wengi kabisa abarani Afrika na inayoongoza kwa kuchimbaji mafuta.

Mwandishi: Hashim Gulana

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman