1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUkraine

Watu 18 wauawa katika ajali ya helikopta nchini Ukraine

18 Januari 2023

Watu wasio chini ya 18 wameuawa katika ajali ya helikopta ya polisi wa Ukraine iliyoanguka kwenye jengo la chekechea nje kidogo ya mji mkuu wa Ukraine, Kiev asubuhi ya leo.

https://p.dw.com/p/4MO6j
Ukraine Kiew - Browary | Absturzstelle Hubschrauber mit Innenminister Denys Monastyrskyj
Picha: Daniel Cole/AP/picture alliance

Watu wasio chini ya 18 wameuawa katika ajali ya helikopta ya polisi wa Ukraine iliyoanguka kwenye jengo la chekechea nje kidogo ya mji mkuu wa Ukraine, Kiev asubuhi ya leo.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Denys Monastyrsky, naibu wake na waziri wa nchi ni miongoni mwa wahanga wa ajali hiyo. Watoto watatu pia wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa. Kulingana na naibu wa mkuu wa ofisi ya rais mjini Kiev, Kyryolo Tymoshenko, helikopta hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea mstari wa mbele wa vita, na uchunguzi bado unaendelea kubainisha chanzo cha ajali.

Viongozi mbali mbali wa Ulaya wametuma salamu zao za rambirambi, huku Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akisema mkasa huo unadhihirisha gharama kubwa inayolipwa na Ukraine katika vita vya uvamizi wa Urusi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema ajali hiyo ni msiba mkubwa.