Watu 17 wauawa na kombora Somalia
14 Desemba 2007Matangazo
Watu 17 wameuliwa na kombora katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Walioshuhudia wanawalaumu wapiganaji wa chini kwa chini wa Kiislamu kwa kuhusika na shambulio hilo.Alhamisi wapiganaji hao walishambulia soko la Bakara.Wapiganaji hao wamekuwa wakipambana dhidi ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Ethiopia.