1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMisri

Watu 16 waokolewa baada ya boti ya utalii kuzama Misri

25 Novemba 2024

Mamlaka nchini Misri zimewaokoa watu 16 baada ya boti ya kitalii kuzama katika pwani ya Bahari ya Sham.

https://p.dw.com/p/4nPdt
Fukwe za Bahari Nyekundu nchini Misri.
Fukwe za Bahari Nyekundu huvutia mamia kwa maelfu ya watalii kila mwaka. Picha: Maksim Konstantinov/Russian Look/picture alliance

Vyanzo vitatu vya usalama vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa oparesheni za uokoaji zinaendelea kutafuta manusura zaidi.

Kwa mujibu wa utawala katika eneo hilo, boti hiyo ilikuwa imebeba watu 45, wakiwemo watalii 31 na wafanyikazi 14.

Gavana Amr Hanasi amesema baadhi ya manusura waliokolewa kwa helikopta na sasa wamepelekwa hospitali. Juhudi za kuwasaka manusura zaidi zinaendelea kwa ushirikiano kati ya jeshi la nchini kavu la Misri pamoja na jeshi la majini.

Bahari ya Sham ni kivutio maarufu cha watalii na ni maarufu kutokana na uwepo wa matumbawe na samaki, ambayo ni muhimu kwa sekta ya utalii ya Misri.