Watu 16 wamepoteza maisha baada ya maporomoko ya udongo kutokea kwenye mji wa Kamituga ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umbali wa kilomita 165 kusini magharibi mwa mji wa Bukavu ndani ya mkoa wa Kivu Kusini. Maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika eneo hilo ambalo ni eneo maarufu lenye migodi ya dhahabu. Sikiliza ripoti ya Mitima Delachance.