1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 12 wauwawa nchini Afghanistan

25 Februari 2012

Waandamanaji 12 wauwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Afghanistan, kufuatia maandamanao ya kupinga kuchoma moto nakala za Quraan kitendo kinachodaiwa kufanywa na vikosi vya majeshi ya kigeni nchini humo.

https://p.dw.com/p/149vV
Vurugu mjini Kabul

Maandamano hayo yaliendelea kwa siku ya nne mfululuzo pamoja na kutolewa wito wa utulivu na rais wa taifa hilo, viongozi wa dini na kuomba radhi kwa rais Barack Obama wa Marekani. Waafghan waliingia mitaan baada ya sala ya ijumaa katika mji mkuu , Kabul pamoja na miji mingine kiasi saba. Jeshi la Marekani limesema kuchomwa moto Quraan ni kitendo ambacho hakikukususudiwa.

Vifo vilivyotokea jana vinafanya idadi ya waliouwawa kufikia 29 mpaka sasa, ambapo inajumuisha pia vifo vya wanajeshi wawili wa Marekani waliouwawa na mtu alievaa sare za polisi wa Afghanistan. Kwa upande wao vikosi vinavyoongozwa na NATO vya jeshi la kimataifa kusaidia kuleta usalama nchini humo, ISAF limesema litafanya uchunguzi wa pamoja na serikali ya Afghanistan kuangalia mazingira yaliyosababisha uharibufu wa vitabu hivyo vya dini.

Kutokana na hali ya kiusalama Ujerumani imefunga kambi yake ya Tolokan iliyokuwepo kaskazini mwa Afghanistan mwezi mmoja kabla ya muda uliopangwa.

Awali kamanda mkuu wa vikosi vya Marekani nchi Afghanistan amevitaka vikosi vyake kujizuia na vitendo vya kulipiza kisasi kufuatia mauwaji ya wale wanajeshi wake wawili yaliyotokana na virugu hizo ambazo kiini chake ni kuchomwa moto kwa vitabu vya dini ya Kiisamu Quraan.

President Barack Obama makes a statement on the tax cut bill at the White House on Monday, Dec. 13, 2010, in Washington. (ddp images/AP Photo/J. Scott Applewhite) // Eingestellt von wa
Rais Barack ObamaPicha: dapd

Kuingia mitaani kwa mara nyingine baada ya sala ya ijumaa kunadhihirisha kushindwa kufanya kazi kwa msamaha huo ulioombwa na rais Barack Obama hapo awali. Mwandamanaji kijana mwenye umri wa miaka 25 mjini Kabul, Kamaluddin alisikika akisema "Hatujali kuhusu msamaha wa Obama". Kijana huyo aliendelea kusema wanapaswa kuwajibika kwa Mungu.

Aidha miongoni mwa viongozi wa dini, Imam Mohammed Magid rais wa Jumuiya ya Kiislamu katika eneo la Amerika ya Kaskazini amesema wameskitishwa sana na kitendo hicho lakini wameipokea samahani iliyotolewa na rais Obama sambamba ahadi ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri: Sekione Kitojo