1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 1,000 wa Pakistan wakamaatwa katika maandamano

27 Novemba 2024

Polisi nchini Pakistan imesema imewakamata karibu waandamanaji 1,000 waliofika katika mji mkuu kutaka kuachiliwa huru kwa waziri mkuu wa zamani aliyeko gerezani Imran Khan.

https://p.dw.com/p/4nUgB
Pakistan Protest
Wanajeshi wakirusha mabomu wa gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha waziri mkuu wa zamani Imran Khan mjini Islamabad, Pakistan, Jumanne, Nov. 26, 2024.Picha: Irtisham Ahmed/AP Photo/picture alliance

Hii ni baada ya maelfu ya watu kufurushwa katikati mwa mji mkuu Islamabad katika msako mkali uliofanywa na vikosi vya usalama. Khan amekuwa jela tangu Agosti 2023, akikabiliwa na kesi anazodai zilibuniwa ili kumzuia kushiriki kwenye uchaguzi mwaka huu uliokumbwa na madai ya wizi. Tangu uchaguzi huo wa Februari, chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf - PTI kimekaidi ukandamazaji wa serikali kwa kufanya maandamano ya mara kwa mara, lakini ya jana ndio yaliyokuwa makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika mji huo mkuu tangu uchaguzi. Zaidi ya waandamanaji 10,000 walimiminika Islamabad, wakikaidi agizo la kupiga marufuku mikusanyiko, na wakakabiliwa na karibu maafisa wa usalama 20,000.