1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 100 wamekufa maji Tanzania kufuatia ajali ya feri

21 Septemba 2018

Idadi ya watu ambao wamefariki dunia kutokana na ajali ya kivuko MV Nyerere imeongezeka hadi 100

https://p.dw.com/p/35ILn
Tansania Fährunglück auf dem Victoriasee
Picha: DW/M. Magessa

Idadi ya watu ambao wameaga dunia kufuatia ajali ya feri MV Nyerere nchini Tanzania, imeongezeka na kupita watu 100.

Waokozi wanaendelea na shughuli zao kutafuta manusura au miili ya watu wanaohofiwa wamefariki.

Kwa mujibu wa ripoti kwenye vyombo vya habari nchini humo, wakati kilipopinduka majini, huenda chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria 200, kiasi ambacho ni maradufu ya kiwango kinachostahili kubeba.

Walioshuhudia wanasema MV Nyerere ilizama wakati abiria walipokimbilia upande mmoja kushuka ilipokaribia kutia nanga.

Kwa mujibu wa mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania Simon Sirro aliyenukuliwa na idhaa inayomilikiwa na serikali TBC Taifa, idadi ya watu waliokufa imeongezeka hadi 100.

Mwandishi: John Juma/AFPE

Mhariri: Lillian Mtono