Watu 10 wajeruhiwa kufuatia maandamano Goma, DRC
20 Desemba 2021Vurugu hizo ni kutokana na maandamano ya mamia ya vijana kutoka makundi ya kiraia waliofunga barabara kadhaa za mji huo wakipinga kuzorota kwa hali ya usalama.
Hayo ni baada ya kutokea kwa mauaji yanayofanywa na watu wenye silaha ambao hadi sasa vyombo vya usalama havijawabaini.
Museveni atetea operesheni ya majeshi yake DRC
Vurugu hizo zilianza pale jeshi la polisi lilipoanza kufyatua risasi za moto kuelekea mamia ya raia vijana walioandamana tangu alfajiri mapema wakipinga kile wanacho kiita uzembe wa vyombo vya usalama kwa kushindwa kuleta amani katika mji huu wa Goma.Nimezungumza na baadhi yao na kwanza wamenaiambia.
Waandamanaji wachoma matairi ya magari barabarani
Katika maeneo kadhaa hususan upande wa kaskazini mashariki mwa mji huu wa Goma, wingu la moshi ndilo limesambaa kote kutokana na matairi yanayo chomwa barabarani na vijana hao ambao wamepinga pia uwezekano wakuingia kwa askari polisi kutoka nchi jirani ya Rwanda kwa lengo la kudumisha usalama kama ilivyo zungumziwa awali na baadhi ya vyanzo kutoka serikali ya Kongo na baadye kusambaa kote katika mitandao ya kijamii.
Rwanda na DRC zachunguza kurudi kwa wapiganaji wa M23
Katika maandamano hayo, watu wawili wameuawa akiwamo afisa wa polisi na wengine wasio pungua 1O wamejeruhiwa kwa risasi za polisi huku shughuli za shule na za kibiashara zikiwa zimefungwa tangu asubuhi.
Polisi ya Congo imeendelea kuwatawanya vijana waandamanaji ambao wameanza kutishia kuekea kwenye ofisi za serikali ili kuziteketeza kwa moto, hali inayo watia wasiwasi mkubwa wananchi.
DRC yakanusha uwepo wa polisi wa Rwanda nchini mwake
Hata hivyo ,akizungumza na DW afisa wa polisi mjini Goma Alisa Job, aliyekuwa kwenye mstari wa mbele katika maandamano amekanusha habari ya kuwasili huko kwa polisi kutoka nchi ya Rwanda katika mji wa Goma na kubaini kuwa ni uvumi mtupu.
Uvumi huo ulikuwa tayari umeenea kwa kasi katika nchi nzima tangu wakuu wa polisi wa nchi hizo mbili kutia saini makubaliano ya kulinda mipaka. Raia wengi wa Kongo waliukosoa mkataba huo wakisema umekosa uwazi. Kwa maelezo kamili,
Katika kipindi cha wiki moja pekee watu zaidi ya 5 waliripotiwa kuawa kwa risasi hapa mjini Goma, mji uliowekwa chini ya utawala wakijeshi mapema mwanzoni mwa mwezi wa mei kwa lengo lakudumisha usalama wa wananchi lakini bila mafanikio hadi sasa.
Umoja wa Mataifa hatiani kuhusu unyanyasaji wa kingono DRC
Mkataba huo ambao umezusha utata mkubwa ulitiwa saini wiki moja iliyopita mjini Kigali, baina ya polisi ya Rwanda na ile ya Kongo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni lengo la kulinda pamoja mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Kwa hivyo polisi wa Rwanda wamejionyesha tayari kuweka kituo chao cha kufanya kazi huko Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Kongo. Jambo ambalo tangu wakati huo limeibua hisia nyingi hapa Kinshasa, haswa ndani ya upinzani.
Baadhi ya wapinzani akiwemo Martin Fayulu, mratibu wa muungano Lamuka, wanadai kuwa huu ni utekelezaji wa mpango wa kuigawa nchi hii. Halafu wametoa wito kwa Wakongomani waikatae polisi ya Rwanda huko Goma.
Polisi ya kitaifa ya Kongo inayo uwezo wa kutekeleza majukumu zake ipasavyo na polisi wana uwezo wa kuwalinda raia wao. Hakuna polisi au hakuna kitengo kinachojiandaa mahali fulani, iwe Rwanda, iwe nchi yoyote kuja kwetu Goma.
Raia hawajui chochote kuhusu undani wa makubaliano ya Kigali
Kinachosababisha mashaka ni kwamba raia hawajui chochote kuhusu undani wa makubaliano ya Kigali na wanaogopa kukabiliwa na matokeo wasiyoyatarajia.
Jacques Sinzahera ambaye ni mwanaharakati wa vuguvugu la wananchi Amka Kongo amekanusha hayo. "Kwa sababu kuna watu ambao tayari walikuwa wameanza kushuku kuwa maafisa wa polisi ya Rwanda watakuja kulinda usalama hapa Goma. Na hivyo vijana wa Kivu Kaskazini kwa ujumla wameyapinga makubaliano hayo yaliyofanywa Rwanda kinyume na katiba yetu. Wakitaka kuingiza jeshi la kigeni ni lazima kusikilizana na wananchi. Jenerali Hamuli hakutueleza yaliyogusiwa huko Rwanda," amesema Sinzahera.
Makubaliano ya kulinda mipaka na polisi wa Kongo na Rwanda yalitiwa saini, huku operesheni za pamoja za jeshi la Kongo na Uganda zikiendelea huko Beni katika mkoa huo huo wa Kivu Kaskazini.