1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wafa, 23 wajeruhiwa kwa bomu la kutegwa Nigeria

18 Aprili 2024

Takribani watu 10 wamefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari lililokuwa likisafirisha wafanyabiashara kukanyaga bomu lililotegwa ardhini kaskazini mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/4ewGj
Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria.Picha: Sunday Aghaeze/AP Photo/picture alliance

Kulingana na vyanzo visivyo rasmi vya kijeshi, tukio hilo lilijiri wakati gari la msafara wa wakulima na wavuvi kutoka mji wa Monguno ukielekea Ziwa Chad lilipokanyaga bomu linaloaminika kutegwa ardhini na wanamgambo wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislam eneo la Afrika Magharibi.

Soma zaidi: Nigeria itawaachia huru watu zaidi ya 300 waliodhaniwa kuwa sehemu ya kundi la Boko Haram

Hata hivyo, jeshi la Nigeria halikutoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali yamerudishwa nyuma kutoka jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambalo walikuwa wakilidhibiti miaka michache iliyopita, lakini bado wanavizia na kulenga misafara inayopita nje ya miji inayolindwa na jeshi.