1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto waliojeruhiwa Gaza kutibiwa nchini Uhispania

Josephat Charo
24 Julai 2024

Ndege ya huduma za matibabu ya jeshi la Uhispania imesafiri kwenda katika mji mkuu wa Misri, Cairo kuwasafirisha watoto hao na vijana wenye umri mdogo, pamoja na wanafamilia 27 hadi Madrid.

https://p.dw.com/p/4igj1
Majeruhi katika Ukanda wa Gaza
Majeruhi katika Ukanda wa Gaza wakipandishwa gari la wagonjwaPicha: Ali Hamad/APA Images via ZUMA Pres/picture alliance

Jumla ya watoto 16 walioko katika hali mahututi kutoka Ukanda wa Gaza watatibiwa katika hospitali za nchini Uhispania. Ndege ya huduma za matibabu ya jeshi la Uhispania imesafiri kwenda katika mji mkuu wa Misri, Cairo kuwasafirisha watoto hao na vijana wenye umri mdogo, pamoja na wanafamilia 27 hadi Madrid.

Soma: WHO: Hospitali za Rafah kukosa mafuta ndani ya siku tatu

Taarifa hii imetangazwa na wizara ya ulinzi ya Uhispania hivi leo ikijibu swali lililokuwa imeulizwa. Wengi wa watoto hao wana majeraha mabaya kutokana na vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza, pamoja na mgonjwa wa saratani mwenye tatizo la moyo. Watoto hao 16 na vijana wadogo waliondolewa kutoka Ukanda wa Gaza na kusafirishwa hadi Misri siku chache zilizopita.