1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto, vijana 9,000 wanyanyaswa kingono katika Kanisa

25 Januari 2024

Ripoti mpya iliyotolewa leo imegundua kuwa watoto na vijana 9,000 wanakadiriwa kuwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono katika Kanisa la Kiprotestanti nchini Ujerumani tangu mwaka wa 1946.

https://p.dw.com/p/4bg0j
Kanisa Kuu la Cologne, Ujerumani.
Kanisa Kuu la Cologne, Ujerumani.Picha: Andreas Rentz/Getty Images

Wachunguzi huru wamesema karibu wahusika 1,259 walifanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya waathiriwa 2,174.

Hata hivyo, idadi ya faili ambazo hazikuchunguzwa inaamaanisha kuwa idadi ya jumla ya waathiriwa huenda ikawa kubwa zaidi.

Soma zaidi: Papa Francis: Madai ya wanawake ni halali kutaka haki zaidi

Chini ya uratibu wa Profesa Martin Wazlawik wa masomo ya kijamii katika Chuo Kikuu cha Hanover, hii ni mara ya kwanza ripoti ya aina hiyo imetoa makadirio ya takwimu za kitaifa na inachunguza sababu za kimfumo za unyanyasaji katika kanisa la Kiprotestanti na uongozi wake.

Kanisa la Kiprotestanti lina karibu wakristo milioni 19.2 wa Kiprotestanti nchini Ujerumani, na kulifanya kuwa jumuiya ya pili kwa ukubwa nchini humo baada ya Kanisa Katoliki.