1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto 19 wafa baada ya kuchomwa moto ndani ya bweni la shule Uganda

Kalyango Siraj15 Aprili 2008

Wengine kadhaa wajeruhiwa

https://p.dw.com/p/DiSF
Wanafunzi wa shule moja ya msingi katika wilaya ya Kiboga nchini Uganda wakiwa darasani. Wenzao 19 wamekufa baada ya kuchomwa na moto uliounguza bweni lao katika shule ya msingi ya Buddo Junior karibu na mji mkuu wa Kampala.Moto ulitokea usiku na chanzo chake hakijajulikana.Polisi inafanya uchunguzi zaidi.Picha: picture-alliance/dpa

Wanafunzi zaidi ya 19 wauwa baada ya kuchomwa na moto uliounguza bweni la shule ya msingi ya Buddo Junior karibu na Kampala,mji mkuu wa Uganda.

Moto uliowauwa watoto hao baado haijajulikana chanzo chake.Lakini mwandishi mmoja wa habari mjini kampala akiwa mahali pale pa tukio ameelza hali katika shule hiyo ikiwa ya huzuni sana.

Chama cha msalaba mwekundu cha Uganda kinajaribu kutafuta mabaki ya watoto walioungua .Mtumishi mmoja wa chama cha msalaba mwekundu ameiambia DW kwa simu kutoka maghali pa tukio kuwa bweni moja lilichomwa kabisa. na walikuwa wakipekuwa vifusi vya bweni hilo kujaribu kutafuta manusura.Anasema kuwa wamepata maiti za watoto kadhaa ambazo zilkuwa zimechomeka vibaya.

Pia wameweza kupta viungo kadhaa vya wanadamu.Ameongeza kuwa bweni moja lilikuwa na watoto 60 na kuongeza kuwa inaonekana kama hakuna hata mtu mmoja alienusurika.

Hali hii inatia shaka habari za awali za wakuu wa shule wanaosema kuwa ni wanafunzi 19 tu ndio waliokufa.

Kwa msasa hawasemi chochote lakini wakati DW ilipowasilina na watu waliokuwa katika sehemu ya tukio wakuu wa shule walikuwa na mkutano na mkuu wa kikosi cha Polisi ya Uganda .

Haikujulikana ni watoto wangapi waliokuwa wamelala katika bweni hilo.Kuna taarifa kuwa milango ya bweni hilo ilikuwa imefungwa kutoka nje na mlinzi wa watoto hao alikuwa hayupo.

Polisi baado inachunguza tukio hilo.

Mwezi machi mwaka wa 2006 takriban watoto 13 waliuawa kwa moto na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati moto ulipounguza shule moja ilioko umbali wa kilomita 300 magharibi mwa jiji la Kampala.