1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watetezi wa haki walaani sera ya uhamiaji ya Ulaya

26 Juni 2023

Watetezi wa haki za binadamu kutoka nchi za Kaskazini mwa Afrika wamelaani sera ya uhamiaji ya nchi za Umoja wa Ulaya, mwaka mmoja baada ya kiasi watu 23 kufariki wakijaribu kuingia kisiwa cha Uhispania cha Melilla

https://p.dw.com/p/4T3im
Spanien | Migranten in der spanischen Nordafrika-Exklave Melilla
Picha: Javier Bernardo/AP/picture alliance

Jukwaa la wanaharakati la eneo la Maghreb, FSMM kuhusu uhamiaji, limetowa malalamiko yao baada ya kukutana katika mkutano wao wa kila mwaka uliofanyika katika mji wa Kaskazini mashariki mwa Morocco wa Nador ulioko karibu na mpaka na Melilla.

Soma pia: Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekubalina juu ya mpango wa kuweka sheria kali za uhamiaji.

Kiasi watu 2,000 wengi wakiwa raia wa Sudan walivamia eneo hilo la mpaka Juni 24 mwaka jana wakijaribu kuingia Uhispania. Kwa mujibu wa Morocco kiasi watu 23 walipoteza maisha. Mkutano huo wa Nador umepitisha azimio la kuukataa mpango mpya wa Umoja wa Ulaya na sera zake za kutaka kuzuia wahamiaji.

Jukwaa hilo limetowa mwito wa kuwepo kile walichokiita, mshikamano wa mataifa na wahamiaji, na kusisitiza kukataa shinikizo la nchi za Umoja wa Ulaya za kuifunga mipaka na kuwafukuza wahamiaji na watafuta hifadhi.