1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WATEKANYARA WADAI PESA:

10 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFtb
TEHERAN: Kwa mujibu wa serikali ya Iran,wale watalii wa Kijerumani waliotekwanyara,huenda ikawa wamezuiliwa na majambazi wanaohusika na biashara ya magendo ya madawa ya kulevya.Majambazi hao wamedai Euro milioni tano. Serikali mjini Teheran imesema itafanya kila iwezavyo kupata uhuru wa mateka lakini haitokuwa na maafikiano yo yote na watekanyara hao.Watalii hao 3 walitekwa nyara walipokuwa matembezoni kwa baiskeli katika jimbo la Sistan- Baluchistan linalopakana na Afghanistan na Pakistan.Wawili kati ya hao watalii ni Wajerumani.