Wateja wa benki ya pili kwa ukubwa Ufaransa watapeliwa Euro billioni 5
26 Januari 2008PARIS:
Polisi nchini Ufaransa wamefanya msako katika makao makuu ya benki ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa ya Societe Generale ambapo mfanya biashara mmoja mhuni, anashutumiwa kwa udanganyifu.Awali benki hiyo ilisema kuwa imemtambua mfanya biashara huyo mhuni ambae alificha hasara ya Euro billioni 5 kwa kipindi cha mwaka mmoja.Mtu huyo alietajwa kama Jerome Kerviel,mfanya biashara wa kiwango cha chini, anashukiwa kutumia uzoefu wake katika benki hiyo kuficha mipango yake ya siri.Pia polisi imefanya msako katika jengo ambalo mtu huyo mwenye umri wa miaka 31 anakoishi.Kervel hajaonekana tangu kashfa hiyo igunduliwe siku ya Alhamisi,lakini familia yake inasisitiza kuwa hana hatia.Wakili wake anasema kuwa mteja wake hajatoroka.Wakati uchunguzi ukiendelea,wachambuzi, serikali ya Ufaransa pamoja na wenye hisa za benki hiyo, wanahoji ni vipi mhuni huyo alivyoweza kufanya mipango yake hio bila ya msaada wa mtu wa nje.
Habari za hivi pundu kutoka Paris zinaeleza kuwa mtu huyo hatimae amekamatwa.