Watayarishi michezo ya olimpiki Tokyo wahakikishiwa viwanja
12 Juni 2020Matangazo
Mkuu wa kamati ya matayarisho ya michezo ya olimpiki mjini Tokyo Toshiro Muto amesema baada ya mkutano wa bodi kuwa wamepata uthibitisho kutoka kwa asilimia 80 ya wale wanaohusika na viwanja hivyo kuwa tunaweza kuvitumia.
Amesema mazungumzo yanaendelea na viwanja vingine , ikiwa ni pamoja na kijiji cha olimpiki.
Watayarishaji nchini Japan wanataka kufanya michezo hiyo kwa njia rahisi kuliko ilivyopangwa hapo kabla ili kuepuka gharama. Wakati huo huo afya ya wanamichezo , maafisa na watazamaji ni muhimu sana kutokana na janga la virusi vya corona.