Watatu wauawa nchini Lebanon
13 Februari 2007Mvua kali ilinyesha huku wakaazi wa Ain Alek walipotazaman mabaki ya mabasi mawili yaliyoshambuliwa na mabomu leo asubuhi na kuwaua watu watatu. Kijiji hiki hicho kilomita 20 hivi kaskazini mwa mji mkuu wa Lebanon Beirat, lakini kile kinachopewa maana katika kesi hiyo ni kwamba wanaoishi katika eneo hili hasa ni Wakristo wanaounga mkono serikali ya Lebanon yenye msimamo dhidi ya Syria na ambao wanapanga kushiriki katika kumbukumbu ya kesho ya kifo cha waziri mkuu wa zamani Rafiq Hariri.
Hariri alifariki miaka miwili iliyopita katika mauaji ambayo Walebanon wengi wanadai yalisababishwa na Syria. Baada ya hapo, kulitokea mfululizo wa mauaji na mashambulizi nchini humo dhidi ya wanasiasa na waandishi wa habari wanaopinga Syria, wanne kati yao kupoteza maisha yao.
Alipotembelea kijiji cha Ain Alik leo asubuhi, mbunge wa zamani wa Lebanon, Nassib Lahoud alisema: “Nadhani, mashambulizi hayo yanalenga kutenganisha raia wa walebanon, kusababisha mivutano na kuvunja nguvu Walibanon katika juhudi zao za kujitegemea. Lakini hatutazuiliwa!”
Mwito huo kwa Walebanon kutoacha juhudi zao za maridhiano uliitikiwa na kwa wanasiasa wengi wa Lebanon leo hii.
Wafuasi wa serikali waliarifu kuwa hawatazuiliwa kufanya maombolezi ya Rafiq Hariri kesho Jumatano licha ya wasiwasi kutokea kwa mivutano na wapinzani wanapiga hema zao kwenye uwanja huo huo wakiandamana dhidi ya serikali. Mtoto wake Rafik Hariri, Saad, ambaye ni kiongozi wa wengi wa wabunge wanaopinga Syria, alithibitisha maombolezi yatafanyika kama yalivyopangwa. Bw. Saad pia alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mahakama ya kimataifa kuchunguza mauaji yaliyofanyika nchini Lebanon. Hadi sasa, upinzani wa Lebanon unaoongozwa na kundi la Hizbollah unachelewesha mahakama haya kuanzishwa ukisema kuwa hautaki mahakama hiyo kuwa chombo cha kisiasa.