Watanzania wanatarajia nini baada ya uchaguzi?
21 Septemba 2020Wakati Watanzania wakishiriki katika uchaguzi wa kisiasa, lengo lao kuu ni kupata fursa ya kuishi maisha bora. Matarajio yao kwa watu wanaochagua kushika madaraka ni kwamba watatoa maoni ya kuboresha zaidi hali za vijiji, miji na sehemu za kazi, kati ya maeneo mengine. Ndivyo anavyosema Anaclet Rwegayura katika Barua kutoka Dar.
Tunafanya uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano. Huu ndio utamaduni wa nchi hii tangu ipate uhuru miongo sita iliyopita. Kumekuwa na maboresho mahimu katika mfumo wa kisiasa na katika mazingira ya mijini, lakini hali ya vijijini haijabadilika sana.
Maeneo ya vijijini bado yana majengo duni ambayo watu huita nyumba zao.
Hii, hata hivyo, sio kiwango cha kawaida cha maisha sehemu zote kwa sababu katika maeneo mengine watu wamejenga nyumba za kisasa, haswa ambapo wana historia ndefu na ya kujivunia kutokana na maisha yaliyofungamana na mashamba ya chakula na mazao ya biashara.
Wilaya yangu, ingawa iko katika moja ya mikoa ambayo mara nyingi huelezewa kama nchi ya neema, bado iko nyuma ya kiwango kinachotarajiwa. Barabara zake bado ni za vumbi kama ilivyokuwa miaka 60 iliyopita. Wanawake na watoto bado wanateka maji kutoka kwenye chemchemi ambazo haziko mbali kutoka nyumbani kwao. Lakini hii haipaswi kuwa sababu ya ukosefu wa usambazaji wa maji ya bomba.
Msitu wa asili ambao ni asili ya kahawa ya robusta, mabwawa mengi ambayo ni sehemu muhimu ya mazingira, aina ya ndege adimu na mapango yenye michoro ya zama za kale havielekei kuvutia macho ya wageni kutoka kote ulimwenguni.
Hizi ni fursa katika kona ya kaskazini magharibi mwa Tanzania ambazo wawakilishi wetu waliopita hawakuwahi kutambua kuwa zinaweza kugeuza mkoa huu kuwa eneo la utalii wa aina yake. Ni wakati sasa wafanyabiashara waliobobea na wenyeji waungane kuwekeza huko na kuuelekeza Mkoa wa Kagera katika masoko ya kisasa ya vitu na huduma mbalimbali.
Serikali yaahidi kuendeleza maisha mapya kuanzia miundombinu hadi umeme.
Akihutubia mkutano ulioweka rekodi katika kampeni yake ya uchaguzi Septemba 16 huko Bukoba, mji mkuu wa mkoa huo, Rais John Magufuli alikiri kupendezwa kwake na mazingira na akasema kuwa atatumia maisha yake baada ya kustaafu huko Kagera.
Serikali tayari imeanza mpango wa kusambaza umeme kwa makazi yote nchini na sasa watu wanapoona safu za nguzo mahali popote, wanasema hizi ni ishara za maisha ya kisasa yaliyoahidiwa. Wamechoka kuishi kizamani. Baada ya uchaguzi, wanatarajia kuendeleza maisha mapya wakiwa na barabara za lami na usiku usio na kiza.
Maendeleo kama haya yatafungua njia za uzalishaji mpya na wakulima wadogo kila msimu watakuwa na malundo ya mazao ya kusafirisha kwenda sokoni. Wagani wa kilimo wa serikali na waganga wa mifugo wataongeza kazi wakiwashauri wakulima kuhusu kupanda mazao na ufugaji badala ya kukaa bure katika vijiji vilivyolala usingizi.
Wanaowania uchaguzi wa serikali za mitaa, ubunge na urais mwezi ujao wapaswa kuzungumza siasa zisizolenga kujenga uchumi wa kisasa ambao ni sehemu ya biashara ya kimataifa.
Biashara za Kitanzania zinahitaji fursa ya kuunda mikondo ya mapato ya ziada.
Inafurahisha kusikia wanasiasa kadhaa wa vyama tofauti wakizungumza juu ya kuunga mkono na kuunda fursa thabiti kwa ajili ya wafanyabiashara wa ndani na nini kifanyike kuinua jamii kwa ujumla. Wote hujaribu kufafanua kile wanachoona kama maendeleo bora ya nchi, japo kwa njia tofauti.
Watu wetu wanahitaji kuelewa kuwa chakula tunachotumia, nguo tunazovaa na bidhaa tunazotumia zinatokana na kilimo. Bidhaa za kilimo ulimwenguni zinazalishwa katika mamilioni ya vishamba vidogo vya familia katika nchi zinazoendelea.
Biashara za Kitanzania zinahitaji fursa ya kuunda mikondo ya mapato ya ziada na kupanuka ili fursa zaidi za ajira zipatikane kwa vijana. Wajasiriamali wanahitaji mwongozo wa wataalam kuzingatia nguvu ya teknolojia ambayo inaendelea kubadilisha vitu vingi ulimwenguni. Je, taifa hili limejiandaa vipi kutumia teknolojia mpya kwa maendeleo yake?
Hakika, kwa kuendelea na amani na utulivu, mustakabali wa Tanzania unaonekana kuwa wa matumainii. Ni kwa sababu hii chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM) kinawahimiza wapiga kura kupuuza wapinzani wake ambao wanafanya kampeni wakipiga ngoma ya utawala wa majimbo kuongoza sera za maendeleo ya nchi. Kwa ukubwa na rasilimali zilizo kila mkoa, hakuna mkoa hata mmoja unaoweza kufikia maendeleo ya maana peke yake.
Kwa hivyo, tunahitaji siasa zisizo za kawaida na wagombea wa uchaguzi watumie majukwaa yao kuhimiza mitandao ya biashara, ambayo itawapa wafanyabiashara nchini fursa ya kuungana na watu wenye nia moja, wakati pia wakisaidia kupata masoko nakutumia teknolojia mpya.
Soma Zaidi: Rais Magufuli aomba kura Mwanza