1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu wa siasa Afrika na Ulaya wakutana Berlin

Harrison Mwilima13 Mei 2022

Wataalamu wa masuala ya siasa barani Afrika na Ulaya walikutana katika bunge la Ujerumani mjini Berlin,kujadili changamoto ambazo dunia inapitia kwa sasa ikiwemo vita vya Ukreine na janga la virusi vya Corona.

https://p.dw.com/p/4BFw6
Josep Borrell I EU sagt weitere Hilfe für Ukraine zu
Picha: Zheng Huansong/Xinua/IMAGO

Mkutano ulioleta pamoja wataalamu na wanasiasa kutoka Afrika na Ulaya, umefanyika jana mjini Berlin katika bunge la Ujerumani. Changamoto za sasa za athari ya vita ya Ukraine na jinsi ya kukabiliana nayo ilijadiliwa.

Wakati nchi mbali mbali duniani zikiendelea kukabiliana na janga la virusi vya corona, vita inayoendelea sasa Ukraine imezidi kuongeza makali.

Hiyo ndio maana majadiliano ya kukabiliana na athari ya vita hiyo ilikuwa ndio dhumuni kuu la mkutano huo unaoitwa the Africa Roundtable au meza ya duara inayojadili Afrika.

Soma zaidi:Umoja wa Mataifa kuamua juu ya uchunguzi Ukraine

Viongozi mbalimbali wa Afrika na Ulaya walihudhuria mkutano huo katika kujadili mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto za sasa.

Ingrid Hamm ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa taasis isiyo ya kiserikali ya Global Perspectives Initiative iliyoandaa mkutano huo. Alisema dunia inakabiliwa na changamoto.

"Tunakabiliwa na changamoto katika kipindi kigumu kama hiki ushirikiano ni kitu muhimu kuliko masuala mengine yote." Aliuambia mkutano

Vita vya Ukraine vyachangia hali ngumu ulimwenguni.

Vita ya nchini Ukraine inayoendelea sasa imesababisha changamoto mbali mbali kama vile upungufu wa chakula na kuongezeka bei za mafuta zilizosababisha mfumuko wa bei.

Bilderchronik des Krieges in der Ukraine | Zerstörung in Mariupol
majengo yalioharibiwa vibaya na majeshi ya Urusi nchini UkrainePicha: Peter Kovalev/TASS/dpa/picture alliance

Nchi nyingi za Afrika huagiza ngano kutoka Urusi na Ukrainena vita ya sasa imesababisha upungufu wa bidhaa hiyo.

Wakati wa hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Kilimo wa Ujerumani, Cem Özdemir, alilaumu vita inayoendelea sasa nchini Ukraine inavyosababisha upungufu wa chakula barani Afrika.

Soma zaidi:Ukraine kusikiliza kesi ya kwanza ya uhalifu wa kivita

"Nchi za Afrika pia zinategemea uagizwaji wa ngano kutoka Ukraine na Urusi. Vita hii inatokea sasa wakati takribani watu milioni 280 barani Afrika wanategemewa kuathiriwa na tatizo la njaa." Alisema na kuongeza

"Changamoto ya njaa inatarajiwa kutokea katika eneo la Sahel na pembe ya Afrika, ambako kuna upungufu wa chakula kutokana na ukame na migogoro" Sehemu ya hotuba yake ilisema.

Afrika sasa inapaswa kutazama upya mifumo yake

Waziri wa Uchumi wa Senegal, Amadou Hott. Yeye alitumia nafasi hiyo kuitisha mabadiliko ya kimifumo ili Afrika iweze kujikwambua katika athari inayosababishwa na vita ya Ukraine.

Mabadiliko hayo yanahusisha kuongeza uwekezaji barani Afrika na kufanikisha urahisi kwa Afrika kupata mikopo nafuu.

Soma zaidi:EU kumimina mabilioni ya Yuro Afrika

Hiyo inawezekana tu kama Afrika ikikaa katika meza ya kufanya maamuzi kama vile kuukubali Umoja wa Afrika kuwa mwanachama wa nchi ishirini zilizoendelea kiuchumi za G20.

"Nchi za Afrika kama kikundi kwa ujumla tunashika nambari nane dunia nzima kwa ukubwa wa mapato yetu ya taifa. Hiyo inamaanisha tunastahili kuwa kama kikundi katika meza ya maamuzi hususani katika kutoa masuluhisho ambayo yanaathiri moja kwa moja bara la Afrika."

Mkutano huo ni wa pili na wa kwanza kabisa ulifanyika mwaka jana na ulijikita katika kujadili chanamoto za janga la virusi vya corona.

Ulaya inawezaje kuwa mshirika wa kuaminika wa Afrika?