1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Sudan Kusini yakaribia kupata mkopo kutoka kampuni ya UAE

18 Mei 2024

Wataalam wa UN wasema Sudan Kusini yakaribia kupata mkopo wa dola bilioni 13 kutoka kampuni ya UAE

https://p.dw.com/p/4g1XR
Konflikt im Sudan | Vertriebene in Gedaref
Picha: -/AFP/Getty Images

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema mkopo huo wa dola bilioni 13 utatolewa na kampuni iliyoko katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), licha ya Sudan Kusini yenye utajiri wa mafuta kushindwa kudhibiti madeni yake.

Jopo hilo la wataalamu limesema katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hati za mkopo ilizopata nakala yake, zinaonyesha makubaliano kati ya Sudan Kusinina kampuni ya Hamad Bin Khalifa, na ambao utakuwa mkopo mkubwa zaidi kuwahi kutolewa.

Ujumbe wa UAE katika Umoja wa Mataifa haukuzungumzia chochote kuhusu makubaliano hayo na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ni ya watu binafsi. Kulingana na mamlaka ya Marekani inayohusika na masuala ya nishati, Sudan Kusini ilizalisha mwaka jana wastani wa mapipa 149,000 ya mafuta.