1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalam: Watetezi wa nishati ya visukuku wasishiriki COP28

1 Novemba 2023

Wataalam wa masuala ya afya kote duniani wametoa wito wa kutowashirikisha kwenye mkutano wa kilele wa hali ya hewa wa COP28, watu wenye ushawishi katika sekta ya mafuta ghafi, makaa ya mawe na gesi asilia.

https://p.dw.com/p/4YGfF
VAE, Abu Dhabi | #COP28 Aufsteller
Mazungumzo ya COP28 mwaka huu wa 2023 yatafanyika DubaiPicha: Amr Alfiky/REUTERS

Wataalam hao wamesema watu hao hawana nafasi katika mazungumzo hayo.

Wito huo umetolewa katika barua iliyochapishwa hii leo na iliyotumwa kwa Rais mteule wa COP28 Sultan Ahmed al-Jaber ambapo wataalam hao wamesema sekta hiyo ya nishati ya visukuku haipaswi kuendelea na kampeni yake ya miongo kadhaa ya kuzuia hatua kuhusu hali ya hewa.

soma pia: Makampuni ya nishati zaidi ya 20 yakubali kupunguza utoaji hewa ukaa

Mwaka jana, mamia ya watetezi wa nishati za mafuta, gesi na maka ya mawe walikilishwa katika mkutano wa hali ya hewa nchini Misri. Mkutano  wa mwaka huu utafanyika huko Dubai kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 12.