Wasoshalisti washinda uchaguzi Uhispania
10 Machi 2008Matangazo
MADRID
Zapatero ameuambia umati mkubwa uliokuwa umeemewa kwa furaha kwamba serikali itafunguwa awamu mpya bila ya mvutano na upinzani wa kihafidhina ambao ulikuwa na sauti bungeni.
Zapatero ameahidi kuongoza kwa kuwafilkiria kabla ya mtu yoyote yule wale watu wasiokuwa na kitu chochote.
Wasoshalisti wamejipatia asilimia 44 ya kura na viti 169 katika bunge lenye viti 350 ikiwa imejiongezea viti kutoka 164 walivyokuwa navyo hapo mwaka 2004 wakati takriban asilimia 99 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa.