Wasiwasi mpya watanda Somalia
16 Desemba 2010Matangazo
Kulingana na wakazi wa eneo hilo waliozungumza na shirika la habari la AFP, hali hiyo ya wasiwasi imesababishwa na uhasama kati ya makundi hayo mawili vile vile wapiganaji zaidi walioongezeka mjini Afgoye.
Kundi la Al Shabab lililo na mafungamano na lile la Al Qaeda limeyateka maeneo mengi ya eneo la kusini na katikati mwa Somalia na mji wa Mogadishu. Wapiganaji wa Hezb al-Islam walio na misingi ya kisiasa zinazoongozwa na Hassan Dahir Aweys, linayamiliki maeneo ya kaskazini magharibi nje ya mji wa Mogadishu vilevile maeneo ya mbali ya kusini mwa nchi.