Mchezo wa soka aghalabu huchukuliwa kama mchezo unaostahili kuchezwa na wanaume tu kutokana na jinsi ulivyotawaliwa na jinsia hiyo kote ulimwenguni. Anapoonekana mtoto wa kike akicheza soka, wengi humtazama kwa mshangao. Lakini sivyo ilivyo katika pwani ya Kenya, kwani watoto wa kike wameuvalia njuga mchezo huu na kwa kweli unawabadilishia maisha yao