1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washutumiwa watatu watiwa nguvuni Istanbul:

16 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0M

ISTANBUL:
Katika taftishi za kushambuliwa mahekalu mawili
ya Kiyahudi mjini Istanbul, Uturuki, polisi
wamewatiwa nguvuni washutumiwa watatu,
viliripoti vyombo vya habari. Wanawake wawili
na mwanamme mmoja walisailiwa na polisi kuhusu
mashambulio hayo ambamo hapo jana waliuawa watu
20 na kujeruhiwa zaidi ya 300, liliarifu
Shirika la Utangazaji N-TV. Nayo magazeti ya
Kituruki yaliripoti kuwa yale magari mawili
yaliyotumiwa katika mashambulio hayo yalijazwa
Tani mbili za miripuko. Pia ilisemekana ziko
ishara kuwa mashambulio hayo yalipangiliwa na
Chama cha Kigaidi AL QAIDA, yaliripoti magazeti
ya Jumapili nchini uturuki. Maafisa wa taftishi
wa Kuturuki wanasaidiwa na mabingwa wa
upelelezi kutoka Israel. Waziri wa Mambo ya Nje
wa Israel Silwan Shalom alifuatana na Waziri
Mkuu wa Uturuki Recep Erdogan, hii leo
waliizuru mojawapo ya mahekalu hayo mawili
yaliyoteketezwa mjini Istanbul na kuwakumbuka
wahanga wa maafa hayo.