1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa 'Dola la Kiislamu' washambulia Libya

29 Oktoba 2018

Watu wanne wameuawa katika mji mdogo nchini Libya kufuatia shambulizi ambalo limefanywa na kundi linalojiita Dola La Kiswahili

https://p.dw.com/p/37Jfq
Irak - Mosul - IS
Picha: Getty Images/AFP/A. Al-Rubaye

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS wameushambulia mji mdogo katikati mwa Libya, na kuwauwa karibu watu wanne, akiwemo mtoto wa kiume wa Meya, na kuchoma moto kituo cha polisi.

Wakaazi wa mji wa Al Fuqaha wamesema leo kuwa shambulizi hilo lilifanyika leo usiku, na kuwa wakaazi kadhaa hawajulikani waliko tangu uvamizi huo, na mpaka sasa hatima yao haijulikani.

Mji huo uko kusini mwa mji wa pwani wa Sirte, ambayo ni ngome ya zamani ya IS.

Shambulizi hilo linadhihirisha namna eneo la katikati mwa Libya lilivyo tete, ambapo IS na makundi mengine yenye silaha, yakiwemo mengine kutoka nchi jirani Chad, yanaendesha harakati zao kwa kuwapora watu kwenye barabara za magari au kushambulia doria za wapiganaji wanaojiita Jeshi la Kitaifa la Libya.