1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washirika wa rais wa Benin wakamatwa kwa kujaribu kumpindua

2 Oktoba 2024

Washirika wawili wa Rais Patrice Talon wa Benin wamekamatwa kwa tuhuma za kupanga mapinduzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/4lL5w
Rais Patrice Talon wa Benin.
Rais Patrice Talon wa Benin.Picha: Séraphin Zounyekpe

Olivier Boko, mfanyabiashara na rafiki wa muda mrefu wa Rais Talon, na waziri wa zamani wa michezo, Oswald Homeky, walikamatwa wiki iliyopita na wako rumande wakingojea kusikilizwa kwa kesi yao. 

Mmoja wa mawakili wa watuhumiwa hao, Ayodele Ahounou, amesema wateja wake wameshtakiwa kwa kupanga njama ya kudhoofisha usalama wa taifa, ufisadi wa fedha za umma na utakatishaji fedha. 

Soma zaidi: Benin yamkamata mkosaji mkubwa wa Rais Talon

Wakili huyo amesema watu hao walikamatwa baada ya kutuhumiwa kumpatia rushwa kamanda anayesimamia idara ya usalama wa rais ili aweze kufanya mapinduzi.

Hivi karibuni, Boko alionesha nia yake ya kugombea katika uchaguzi wa urais wa Benin mwaka 2026. 

Wakosoaji wanamshutumu Rais Talon kwa kutumia mfumo wa mahakama kuwashambulia wapinzani wake kisiasa, tangu alipochukuwa madaraka mwaka 2016.