1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:ziara ya Kansela Schroeder Marekani

27 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzR

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amejiandaa kukutana na rais Gorge Bush wa Marekani mjini Washington.

Mada zinazotarajiwa kuhodhi mkutano huo ni juu ya hatma ya Umoja wa Ulaya,msaa kwa nchi maskini pamoja na mzozo juu ya mageuzi kwenye Umoja wa Mataifa.

Bwana Schroeder anatarajiwa kutilia mkazo juu ya ombi la Ujerumani la kutaka kiti cha kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Marekani imekataa kuiunga mkono Ujerumani kupata kiti cha kudumu kwenye baraza hilo.

Katika hotuba yake kwa baraza la biashara la Marekani bwana Schroeder ametaka kuwepo uhusiano mkubwa wa kibiashara kati ya nchini hizo mbili.

Kansela huenda akakumbana na uchaguzi wa mapema ambapo kura ya maoni tayari imemuonyesha kushindwa iwapo uchaguzi huo utafanyika mwezi septemba.